Posts

Showing posts from February, 2023

Mambo Ya Ajabu Yaonekana Kwenye Kuaga Maiti 12 Za Ajali Iliyoua 20 Tanga

Ni msiba juu ya msiba. Yanakosekana maneno ya kutafsiri kilichotokea katika viwanja vya Hospitali ya Huruma, Wilaya ya Rombo ambako lilifanyika zoezi la uagaji miili ya watu waliokufa katika ajali kule mkoani Tanga, ndugu walikua wanaanguka na kuzimia uwanjani hapo wakati maiti za wapendwa wao zikiwa kwenye majeneza, Mwananchi imeripoti. Ajali hiyo ilitokea Februari 4 usiku katika eneo la Magira Gereza, Kata ya Magira Gereza, Wilaya ya Korogwe, barabara ya Segera- Buiko mkoani Tanga. Na imesababisha vifo vya watu 21 mpaka sasa, huko mmoja kati ya hao- akiwa ni marehemu aliyekua akisafirishwa kwa mazishi kule Moshi. Ndugu na majirani waliambatana viwanjani hapo kuaga miili ya ndugu zao wa ukoo mmoja, waliofariki ajalini wakiwa katika zoezi la kuusindikiza mwili wa Athanas Mrema aliyekua na miaka 59. Athanas alifariki Februari Mosi na mazishi yake yalipangwa kufanyika kule Moshi, ambapo ajali hiyo ilipatikana wakati wa safari ya kuusafirisha mwili wake. Kwenye mazishi ambayo yamefanyika ...